Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani katika Mji Mdogo wa Mirerani, Simanjiro Mkoani Manyara, alipokea zawadi ya pete iliyotengenezwa kwa dhahabu nyeupe na kidani cha Tanzanite kwa niaba ya Mke wake Mama Mary Majaliwa, kwa makubaliano na Mkewe aliamua kuikabidhi pete hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ili iuzwe na fedha zitakazopatikana zitumike kujenga mabweni kwa ajili ya watoto wenye uhitaji katika wilaya ya Simanjiro.