Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutokana na itilafu ya mtandao.
Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ilipangwa kuendeshwa kwa njia ya mtandao “Video Conference” lakini ikashindikana kutokana na tatizo la kimtandao.
Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala amesema kutokana na sababu hizo, Mbowe atafikishwa Mahakamani August 6, 2021 badala ya kesi hiyo kuendeshwa kwa njia ya mtandao. Mbowe alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza July 26, 2021 kwa mashtaka mawili ikiwemo la tuhuma za Ugaidi
Hapa nimekusogezea video ujionee Mfuasi wa Chadema akiingizwa kwenye Gari la Polisi kisha Wakili Kibatala aingilia kati na kumwambia “Tutakutoa tu”
MTANDAO WAKWAMISHA KESI YA MBOWE, MAHAKAMA YATOA MAELEKEZO “WALIOKAMATWA TUNAWAFUATILIA”