Club ya Simba SC leo kupitia CEO wao Barbara Gonzalez imetangaza kuingia mkataba wa udhamini wa miaka miwili na kampuni ya bima ya MO Assurance ambapo itawezesha Simba SC kuanzia wafanyakazi wake na wachezaji wa timu zote za Simba kupata bima ya afya.
Mkataba wa huo una thamani ya Tsh milioni 250 kwa mwaka nje ya gharama za matibabu watakazokuwa wanalipa MO Assurance na bima hiyo ya afya itatolewa kwa mchezaji/mfanyakazi wa Simba SC na wategemezi wake wanne (mke/mume na watoto watatu).
Mwaka jana tu Simba SC imeingia gharama ya kutoa zaidi ya Tsh milioni 300 kwa ajili ya matibabu kwa wachezaji wake kitu ambacho baada ya mkataba huo sasa MO Assurance ndio watakuwa wanalipia kupitia bima yao #MillardAyoSPORTS