Ni April 4, 2022 ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum limewakamata wahutumiwa waliokuwa wakijaribu ama kuhujumu miundombinu ya Daraja la Tanzanite Dar es Salaam.
Akizungumza na Vyombo vya Habari Kamanda wa Polisi Jumanne Muliro anasema wahutumiwa hao wamekamatwa baada ya kukutwa wakijaribu kufungua baadhi ya vyuma na kutaka kuchukua kwaajili ya shughuli zao binafsi.
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani Aidha Jumanne Muliro amewataka Wananchi kutunza miundombinu na endapo uhalifu unapotokea basi usisite kutokea taarifa mapema katika kituo chochote cha Polisi.
TAZAMA WAWILI WALIVYOKAMATWA WAKIJARIBU KUFUNGUA NA KUIBA VYUMA DARAJA LA TANZANITE