Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) limesitisha huduma za usafiri kati ya New Kapiri-Mposhi na Kasama Zambia ili kuruhuru ukarabati kwenye daraja la Chambeshi ambalo liliharibika kutokana na ajali ya gari moshi ya mizigo iiyotokea Mei 13.
Katika kipindi cha wiki 12 cha ukarabati, vituo vya Chambeshi na Kasama vitafungwa kwa treni za abiria ili kuepusha madhara abiria. Taarifa iliyotolewa na Tazara imesema huduma zitaendelea kati ya Kasama na Nakonde.
“Katika kipindi hicho, mabehewa ya mizigo yatakuwa yakisukumwa kuvuka eneo hilo la daraja ili mizigo iendelee kupita kutoka Kapiri-Mposhi,” Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma wa Shirika, Conrad Simuchile.