Habari za Mastaa

Flora Mvungi kaongea kuhusu wanaosema ameachana na H Baba

on

Miongoni mwa stori zilizo-make headline kwenye mitandao siku za hivi karibuni ni pamoja na stori iliyosambaa ikidai kuwa ndoa ya mastaa wa Bongofleva, Hamis Ramadhan ‘H Baba’ na mwigizaji Flora Mvungi imevunjika huku wengine wakisema H Baba amehama nyumbani kwenda kuishi hotelini.

Kupitia The Weekend Chart Show SHILAWADU’ ya Clouds TV July 28, 2017 kulikuwa na stori kwamba H Baba anaishi hotelini na Flora amerudi nyumbani kwao baada ya ndoa yao kuvunjika na walimtafuta Flora Mvungi ili kujua ukweli ambaye alibainisha kuwa hawajaachana na wanaishi vizuri na mume wake.

>>>”Mimi sina taarifa hizo, sijaachana na mume wangu. Kwanza nani kasema hizi habari? Sijaachana na mume wangu, sasa tatizo linatoka wapi? Tupo naye tunakaa wote vizuri tu. Kwani leo ukiwa na mkeo mkaamua kwenda kulala hotelini kuna tatizo?

“Siyo kweli mbona hata ada ya Chuo yeye ndiye ananilipia. Haishi hotelini, tunaishi naye. Ataishi vipi hotelini wakati naishi naye? Kwanza akisikia atashangaa sana mimi nakaa na mkwe wangu kweli na sijaachana na mume wangu. Hizi habari kwanza ndio nazisikia kwenu. Sijui kama anishi hotelini ila najua kama yupo kwenye kazi zake.” – Flora Mvungi.

TANZANIA KIDS GOT TALENT! Shindano la Watoto wenye vipaji Tanzania 

Soma na hizi

Tupia Comments