Top Stories

CCM Tabora kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Uyui aliyemuomba Rais Magufuli kuacha kazi

on

Imetokea kwenye wilaya ya Uyui Tabora Tanzania ambako taarifa za January 26 2017 zilianza kusambaa kuwa mkuu wa wilaya hiyo Gabriel Mnyele amejiuzulu.

Mnyele alipohojiwa na millardayo.com jioni ya January 26 Mnyele hakutaka kuweka wazi kama ilivyosemekana kwa kusema ‘nimekasirika kwa hizo taarifa sababu watu wananichuria na kuniondolea muda wangu ambao naupenda, just imagine mpaka mke wangu amenipigia kuniuliza kama ni kweli, ingekua kweli basi ingetangazwa tu na mamlaka’

AyoTV na millardayo.com hazikuishia hapo zikampata katibu wa CCM Tabora aliyesema >>> ‘Mnaweza kuwa mmelipokea vibaya kwamba amejiuzulu, taarifa alizotupa sisi na alipokua ofisini kwangu ni kwamba aliandika barua kumuomba Rais mapema nadhani zaidi ya mwezi mmoja uliopita

Mheshimiwa Rais kwa taarifa zake za kwamba amemkubalia toka jana kwamba anamkubalia nafasi hiyo aiache wazi ambapo mimi baada ya kupata taarifa hiyo maana ni sehemu ya Kada wangu maana ninafanya nae kazi siku hadi siku, nikamuita na akatueleza na kutuaga‘ – Katibu wa CCM Tabora

Tukamuuliza mbona imekua mapema hivi? akasema hapana ni kwasababu ya shughuli zangu nilikua nimemuomba Rais……….. maana kabla ya kuwa mkuu wa Wilaya alikua ni Wakili wa kujitegemea hivyo kesho anaondoka anarudi Dar es salaam mpaka atakapokua ameteuliwa mwingine nitakuja kumkabidhi ofisi

UNAWEZA KUSIKILIZA ZAIDI HII SAUTI HAPA CHINI KWA KUBONYEZA PLAY

AUDIO: Sikiliza hapa chini Mahojiano na Mkuu wa wilaya aliyeacha kazi Uyui Tabora.

Soma na hizi

Tupia Comments