Top Stories

Mwanri avunja watu mbavu, amwambia Waziri Mkuu “sauti hii ni msisitizo tu Mkuu wangu sikugombezi” (+video)

on

Ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akiongea mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim huko Tabora kwenye jukwaa la kufungua fursa za kibiashara kwa Mkoa huo,

Mwanri alimwambia Waziri Mkuu, “Mkuu niombe niseme neno moja ambalo litaogopesaha watu lakini kama ni noma na iwe…. hapa tumefungua Viwanda ulinisaidia Mkuu tumekwenda mpaka Manonga ambayo ilikua haifanyi kazi miaka 20 iliyopita sasa inafanya kazi, ule umeme ulioagiza uende pale umekwenda na kuna ajira pale”

“Ulipokuja mara ya mwisho hapa Tabora tulikupeleka katika kiwanda cha TABOTEX na tukaahidiwa kwamba mwezi wa kumi na mbili kiwanda kile kitakua kinafanya kazi na watu wa TABOTEX nimewaita hapa na nimesema waitwe hapa kwa sababu sitaki nionekani nimekuja kuwasengenya au kuwateta”

Ikifika January tarehe moja Mh. Waziri Mkuu…. sauti hii ni msisitizo tu Mkuu wangu kwamaana mimi siwezi kukugombeza wewe, ikifika January moja kama Kiwanda kile kitakua hakifanyi kazi, nitachofanya ni kuandika barua kwako kukushauri kirudishwe Serikalini ili tutafute Mwekezaji Serious katika Mkoa wa Tabora” – Agrey Mwanri

Bonyeza play hapa chini kumtazama Mkuu wa Mkoa Mwanri akiiongelea hii ishu mwanzo mwisho…….

VIDEO: RC WA SUKUMIA NDANI ALIVYOVUNJA WATU MBAVU MBELE YA WAZIRI MKUU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments