Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imenyakua tuzo tatu katika usiku wa utoaji wa tuzo za Mwajiri Bora zilizofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2024.
Katika usiku huo wa tuzo TCAA imenyakua tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Maudhui ya Ndani, Tuzo ya mshindi wa pili ya Mwajiri Bora katika Sekta za Umma na Tuzo ya jumla ya Mwajiri na Mtendaji Bora.
Tuzo hizo zimekabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko aliyekuwa Mgeni rasmi, akiambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Tuzo hizo huandaliwa kila mwaka na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) lengo likiwa ni kushindanisha taasisi mbalimbali katika nyanja za usimamizi bora wa rasilimali watu mahala pa kazi.