Mix

TCU yatoa sifa mpya kujiunga na vyuo vikuu

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii ya kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘TCU YATOA SIFA MPYA KUJIUNGA VYUO VIKUU’

Gazeti hilo limeandika kuwa Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU‘ imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi  wakiwa hatarini kukosa nafasi ka kukosa sifa na vigezo.

Utaratibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Sifa hizo zilizowekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa jana, Moja ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo ni wahitimu wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa ‘D mbili’ pointi 4.0. Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokan na ufaulu wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1.

Taarifa hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 ili wawe na sifa za kudahiliwa z, watatakiwa kuwa na alama za ufaulu wa ‘C mbili’ pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B+=4; B=3; C=2; D=1.

Kupitia tovuti hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu watahitajika kuwa na ufaulu wa alama ‘D mbili’ 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1.

Mbali na sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne ambazo ni D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F=0-38.

Sifa nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na baraza ka Taifa la mitihanai ‘NECTA’ na mafunzo ya ufundi ‘VETA’ 

Watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.

Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udaahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA. 

SOURCE: Gazeti la Mtanzania

Unaweza kuzipitia habari nyingine hapa chini kwenye magazeti ya leo 

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 17 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments