Leo April 24, 2018 Shahidi wa kwanza katika kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kuwa katika maelezo ya Tido alikiri kusaini mikataba na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila kumshirikisha mtu yeyote.
Shahidi huyo ambaye ni Afisa wa uchunguzi mwandamizi wa TAKUKURU, Victor Malaki mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi alidai kuwa Tido alikiri hayo wakati alipokuwa anachukuliwa maelezo ya onyo.
Akiongozwa katika kutoa ushahidi wake na Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai, Malaki edai kuwa alianza kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za mshtakiwa kusaini mikataba na Channel 2 Group Corporation (BV1) ya urushwaji wa matangazo kutoka Analogia kwenda Digitali bila kumshirikisha mtu na kwamba hakufuata sheria ya manunuzi ya umma mwaka 2012
“Kabla ya kusaini mikataba hiyo walikuwa na mazungumzo na Mwenyekiti wa channel 2 Ajai Set ambapo Tido alisema mikataba hiyo haijakamilika na nia ya kusaini ilikuwa ni kuisaidia serikali kuhama kwenye matangazo analogia kwenda Digitali” amesema Swai
Alidai kuwa mikataba hiyo aliisaini Tido Mwenyewe bila kufuata taratibu na kupelekea TBC kufunguliwa shauri la madai huko Uingereza kutokana na mikataba hiyo.
Shahidi huyo amedai kuwa Tido alisababisha hasara ya Sh. Milion 887.2 kwani TBC ilishindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba huo na kusababisha Channel 2 kufungua kesi huko Uingereza ambapo serikali ilimlipa mwanasheria ili kuitetea TBC.
September 7,2012 Tido alikuchuliwa maelezo ambapo alikuwa na wakili wake Jesse na baada ya maelezo alisaini kuthibitisha maelezo yake.
Baada ya ushahidi huo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi April 24,2018 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi
Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili, anadaiwa kuwa June 16, 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.
GWARIDE: Lilivyokaguliwa na Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli Dodoma