Duniani

Sio lazima nyumba ya matofali, Teknolojia inakupa na nyumba ya mtindo huu!! (Pichaz)

on

Ukimwambia mtu yoyote kwamba unatafuta vifaa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yako, moja kwa moja mawazo ya watu wengi ni kwamba nyumba yako inahitaji mawe, mchanga, cement na vitu vingine kama hivyo… lakini moja ya stori ambazo millardayo.com huwa inakuwekea ni story zenye vitu tofauti na ilivyozoeleka.

Ukiachana na story ya nyumba iliyotengezwa kwa Makontena, nyumba za mbao na vioo, uko na huu ubunifu ambao kiukweli ni wa kuvutia sana ambao Jono Williams amebuni toka New Zealand, Mjengo wake kaupa jina la Skysphere na imemchukua miaka mitatu tu mpaka kila kitu kukamilika.

Hizi pichaz ni hatua za kwanza kwenye ujenzi wenyewe.
150730150232-skysphere-construct-super-169

150730150755-skysphere-woods-super-169

Mambo yakaendelea vizuri, ujenzi unasogea tu kwenye hatua ya kukamilika.

150730151447-skysphere-work-super-169

150730141619-skysphere-solar-super-169

Juu ya mjengo kuna panel za Solar kwa sababu umeme unaotumika kwenye nyumba ni umeme wa nguvu ya jua (Solar Power).

Ujenzi umefikia pazuri, Time ya kuona na vitu vya ndani mtu wangu.

150730141945-skysphere-bed-super-169

Karibu mgeni, hapo ndio ambapo jamaa ameweka kitanda chake poa kabisa cha kumtosha yani !!

150730142547-skysphere-cave-super-169

Upande mwingine ni huu ambao jamaa kaweka sofa yake poa kabisa pamoja na Flat Screen yake kwa juu.

150730144723-skysphere-blue-super-169

Kilichotumika kwenye ujenzi wote ni mabomba ya chuma na upande wa ukuta ni kioo kitupu ukiwa ndani unaona kila kitu kinachoendelea nje.

  150730143845-skysphere-steps-super-169   150730151205-skysphere-beer-super-169

Kwanza kabisa hii nyumba kila kitu kimeunganishwa na system ya App ambayo mwenye nyumba yuko nayo kwenye simu yake, unaambiwa hata kama vinywaji vimepungua kwenye fridge hana haja ya kufunua kuangalia, App ya kwenye simu yake inampa majibu yote.

150730150943-skysphere-app-super-169

Hii ndio App yenyewe mtu wangu, kama kuna mlango uko wazi, nini hakipo kwenye friji, kuwasha na kuzima taa, vyote unavijua kupitia kwenye simu yako.

150730152339-skysphere-exterior-super-169

Jono Williams anasema mpaka ujenzi umekamilika imemgharimu kiasi cha Pesa ambacho ni zaidi ya Dola 50,000 ambazo kwenye Tshs inagusa juu ya Milioni 108.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments