Naibu katibu Mkuu Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Prof Daniel Mushi amesema ili nchi ipige hatua kimaendeleo ni lazima kutumia tenkolojia ambayo inamchango mkubwa Katika kuleta mabadiliko nchini na duniani kwa ujumla.
Porofesa Mushi ameyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la tatu la kimataifa la vyuo vya elimu ya juu vya ndani na nje ya nchi lililoandaliwa na Chuo kikuu Mzumbe ambapo amesema teknolojia ikitumika vizuri inaweza kusaidia kupiga hatua kwa Kasi kubwa na endapo haitatumika vizuri inaweza kuharibu vizazi vya sasa na vijavyo.
Amesema kwa Sasa dunia nzima inatumia tenkolojia ya akili mnemba (AI) hivyo Tanzania ni nchi kama nchi zingine duniana lazima tuhakikishe tunakuwa miungoni Kwa wanufaika kupitia tenkolojia mbalimbali ambazo zinakuwepo Duniani.
Kwa upande wake makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof William Mwegoha amesema ulimwengu unabadilika sana na kueleza muktaza wa dhana ya taaluma za maendeleo na changamoto mbalimbali hivyo taaluma za maendeleo ni muhimu kupitiwa ili ziweze kuendana na mabadiliko ya dunia kwa kuwa ni umuhimu.
Amesema kama Chuo licha ya Kutoa elimu na taaluma mbalimbali katika Chuo hicho Kwa wanafunzi pia wanahakikisha wanafunzi wanapata elimu ya ujasirimali ambao unaenda sambamba na matakwa na soko la Dunia Ili kuwakomboa kiuchumi.
Naye Prof. Elizabeth Genda mkurugenzi wa Taasisi ya maendeleo chuo kikuu Mzumbe amebainisha kuwa hili ni jukwaa muhimu kujadili mchango wa maendeleo ya taaluma katika kuboresha maisha ya watu.
Kongamano hilo la tatu la kimataifa linafanyika kwa siku mbili kuanzia disemba 10 na kumaliza disemba 11 mwaka huu ambapo huandaliwa na vyuo mbalimbali ambapo mwaka huu limenadaliwa na Chuo kikuu Mzumbe huku vyuo vingine vilivyoshiriki ni Panola na Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo(SUA),Chuo kikuu cha Afya Muhimbili(MUHAS)Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam(UDSM).