Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ndiye mgeni rasmi katika Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yatakayofanyika mjini Geita Mkoani Geita kuanzia tarehe 20 hadi 30 Septemba, 2023 katika Uwanja wa EPZ- Bombambili.
Maonesho haya yatafunguliwa tarehe 23 September na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko (Mb) huku Mgeni Rasmi akiwa Rais Samia September 30 2023 ambapo kauli mbiu ni “matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua Wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira”
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita kwa kushirikiana na TANTRADE na halmashauri ya mji Geita imesema kila mtu anakaribishwa kwenye maonesho haya na hakuna kiingilio chochote hivyo Wananchi au wenye Vyombo vya usafiri wanakaribishwa “tunawakaribisha sana na pia mnaweza kuwasiliana nasi kwenye 0758-18-00-13″