Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imewahukumu kifungo cha kila mmoja miaka 20 jela Zebedayo Safari (34) na John Daffi (42) Wakazi wa Endagile Babati kwa kosa la uhujumu uchumi baada ya kukutwa na meno mawili ya Tembo.
Washtakiwa hao walikamatwa October 23, 2022 katika Kijiji cha Bulkeri ambapo kila mmoja alikutwa na jino moja la Tembo kwenye mfuko ambapo ni sawa na Tembo mmoja huku thamani yake ikiwa ni zaidi ya Tsh. Milioni 35 kwa wakati huo.
Washtakiwa hao walikamatwa wakati Askari wa TANAPA wakiwa doria baada ya kupata taarifa kutoka kwa Raia mwema kuwa Washtakiwa hao wamebeba meno ya Tembo ndipo wakaweka mtego na kuwakamata wakiwa kwenye usafiri wa bodaboda na baada ya kuwekwa chini ya ulinzi dereva wa bodaboda aliweza kutoroka.
Upande wa utetezi wa Washtakiwa hao umeiomba Mahakama kuwapunguzia adhabu huku mmoja akisema Mama yake ni Mzee, Das yake ni Mlemavu na ameachiwa Watoto wadogo na wote wanamtegemea yeye.