Ikulu ya White house imetoa wito juu ya kuongeza udhibiti wa bunduki nchini Marekani baada ya tukio la kijana wa miaka 28 kufyatua risasi katika shule ya msingi ya Kikristo huko Nashville, na kuua sita, wakiwemo watoto watatu.
“Wakati umekuwa katika chumba hiki, sijui kama umepitia kwenye simu zako, lakini tushuhudia kuhusu ufyatuaji risasi mwingine huko Tennessee ufyatuaji risasi shuleni na sina neno,” Alisema mke wa Rais Jill Biden katika hafla moja huko Washington wakati ripoti za kupigwa risasi katika Shule ya Covenant zilianza kusambazwa.
“Watoto wetu wanastahili mafundisho bora zaidi na tunasimama, sote, tunasimama na Nashville katika maombi,” aliongeza.
Rais Joe Biden pia alihutubia kuhusu tukio hilo la ufyatulianaji risasi wa shule mara baada ya hapo, akarudia wito wake kwa Congress kuchukua hatua za kisheria.
Biden aliita upigaji risasi “huvunja moyo, na huwa ni ndoto mbaya zaidi ya familia”. Alisema mengi zaidi yanafaa kufanywa ili kukomesha ghasia za utumiaji bunduki.
“Matukio haya yanaharibu jamii zetu,” alisema, na kutoa wito kwa Congress kupitisha marufuku ya matumizi silaha akisema “tunahitaji kufanya zaidi kulinda shule zetu”.
Mapema mwezi huu Biden alitangaza muongozo mpya wa hatua za kiutendaji zinazolenga kupunguza ghasia za bunduki na kuenea kwa bunduki zinazouzwa kwa watu waliopigwa marufuku.
Hatua hizo zililenga kuimarisha ukaguzi,kukuza uhifadhi salama zaidi wa silaha na kuhakikisha vyombo vya kutekeleza sheria vinaenenda kwa sheria ya udhibiti wa bunduki ya pande zote mbili iliyopitishwa msimu wa joto uliopita.
Lakini hatua zake hazikubadilisha sera ya serikali, lakini badala yake zilielekeza mashirika ya shirikisho kuhakikisha kufuata sheria na taratibu zilizopo.