Michezo

Kama ilikupita ile stori ya uwanja wa tennis wa kuvutia Dubai nimekuwekea hapa (+Pichaz)

on

Huenda ukawa umesikia stori nyingi kuhusu Dubai ila hii ikawa ilikupita, Dubai ni moja kati ya sehemu zinazoongoza kuwa na majumba ya kifahari hoteli nzuri, karibia kila kitu kilichomo ndani ya Dubai ni kivutio kwa wageni kutoka nchi nyingine, hata gari za polisi za Dubai ni gari ambazo za thamani kubwa.

a

Ni kawaida kwa Dubai kuona Ferrari, Lamborghini na magari mengine ya kifahari kutumika kama magari ya polisi wakati kwa nchi nyingine hutumiwa na watu matajiri sana na wenye kipato kikubwa. Sasa hii ni stori nyingine tena ya kuvutia kutoka Dubai kuhusu mchezo wa tennis.

9

Dubai ndio sehemu pekee kuna uwanja wa tennis mrefu kuliko yote wa kuvutia, mrefu kwa maana umejengwa juu ya ghorofa, ila stori sio tu kuwa juu ila ni namna ambavyo umejengwa katika hoteli inayotajwa kuwa ya nyota saba duniani Burj Al Arab.

Flying_Tennis_Court_at_Burj_Al_Arab_Dubai_CM3-e1312245482812

2

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments