Michezo

Ushindi wa mastaa hawa wa tennis katika mashindano ya dunia ukufikie…

on

Nyota wa mchezo wa kikapu duniani Roger Federer Novak Djokovic wameendelea kuonyesha wao ni bora zaidi duniani katika mchezo huo baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya wanaume ya tenisi ya dunia.

Federer alianza kwa kushinda seti ya kwanza kwa 7-5 kisha akapoteza seti ya pili kwa 4-6 kisha akamaliza kwa ushindi wa seti 6-4, dhidi ya Kei Nishikori wa Japan

Kwa upande wa Novak Djokovic ambaye anashikilia rekodi ya kuwa namba moja kwa uboraduniani aliendeleza wimbi la ushindi katika michuano hiyo kwa kumchapa Tomas Berdych.

Djockovic alipata ushindi wa seti mbili ambapo seti ya kwanza alishinda kwa 6-3 na kisha akamaliza kwa ushindi wa 7-5.

Kwa matokeo hayo kesho Jumamosi Djokovic atachuana na Rafael Nadal  huku Roger Federer akimsubiri mshindi wa leo kati ya Andy Murray au Stan Wawrinka katika hatua ya nusu fainali.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments