Habari za Mastaa

Tessy afunguka kuhusu bidhaa zake ‘Nashukuru bidhaa zinafika mpaka Marekani’

on

Ni  Mrembo na Mjasiriamali  Kayitesy Abdul maarufu kama Tessy Chocolate ambae kwasasa anaingia kwenye orodhaa ya vijana waliojiajiri na kutoa ajira kwa vijana wenzake kupitia biashara yake aliyoanza tangu April 23 mwaka 2020.

Kwa Mujibu wa mrembo huyo anasema biashara hiyo ya uuzaji wa bidhaa zake Momo Beauty Product zimemletea wateja mbalimbali wakiwemo waliopo nchini na hata nje ya Tanzania.

.

Tessy akizungumza na millardayo.com anasema ‘Namshukuru sana Mungu pili nitoe shukrani zangu kwa wateja wangu wanaonunua bidhaa zangu,sasa hivi biashara yangu ya Momo Beauty Product inawafikia mpaka watu waliopo Marekani, Canada, Kenya, kiufupi hizo nchi zina mawakala wangu’– Tessy

.

Miongoni mwa mipango yangu kupitia hii product ni kuendelea kuunga mkono Serikali ya awamu ya Sita ya Rais, Samia Hassan Suluhu kwa kutoa ajira kwa vijana wenzangu hiyo ndio mipango ya kufungua kampuni kubwa ambayo itatoa ajira kwa vijana wenzangu zaidi ya 50 na kuendelea’ Tessy Chocolate

‘Kwasasa  Ofisi zangu zinapatikana Sinza Kijiweni Dar es Salaam ama unaweza kuwasiliana na  mimi mwenyewe 0675 718718 ukinipigia nakuhudumia bidhaa zangu za Momo Beauty Product’- Tessy Chocolate

.

TESSY KAFANYA HILI BAADA BIASHARA YAKE YA MWANZO KUVAMIWA, KAFUNGUKA YOTE

Tupia Comments