Top Stories

Tetemeko la ardhi lapiga Uturuki

on

Tetemeko la Ardhi lililotokea mchana wa Ijumaa ya tarehe 30 Oktoba 2020 katika Ukanda wa Bahari ya Aegean limeharibu miundombinu katika Miji ya Pwani.

Watu katika Mji wa Izmir uliopo Magharibi mwa Uturuki, wamekusanyika katika mitaa baada ya kuyakimbia majengo yao wakitafuta usalama. Meya wa Mji huo amethibitisha kuwa takriban majengo 20 yameharibiwa.


Taarifa zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Suleyman Soylu kupitia mtandao wa ‘Twitter’ ni kuwa Miji mingine iliyoharibiwa na tetemeko hilo ni Bornova, Bayrakli.

Aidha, Waziri Suleyman Soylu ameongeza kuwa Uchunguzi bado unaendelea katika eneo hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa takriban watu wanne (4) wamefariki huku 120 wakiwa wamejeruhiwa kufuatia Tetemeko hilo.

UAMUZI WA TCU BAADA YA KUPOKEA MAOMBI “UDAHILI UMEKAMILIKA, VYUO 74, WAOMBAJI ELFU 98”

Soma na hizi

Tupia Comments