Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.7 Kipimo cha Richa limetokea karibu na Mji wa Sivrice, Mashariki mwa Mkoa wa Elazig na kuua takriban Watu 6 hadi sasa pamoja na kujeruhi takriban Watu 225.
Majengo mengi yameharibiwa kutokana na tetemeko hilo linaloelezwa kuwa na Kina cha Kilometa 10 kwa mujibu wa Shirika la Kijiolojia ambapo Watu takriban 500,000 walilisikia tetemeko hilo.
Aidha, matetemeko 15 baada ya tetemeko hilo kuu yamesikika pia katika Mataifa Jirani kama Iraq, Syria na Lebanon.