Mix

Mzazi kakatisha uhai wa watoto sita, kisa ni amri za MUNGU kukiukwa na mtoto wake…

on

DAVID4

.

Stori inasikika kutoka Texas Marekani, inamhusu mwanaume mmoja aliyeamua kukatisha maisha ya watoto 6, mmoja ya watoto wao ni mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 13 !!

David Conley amekamatwa kwa kesi ya mauaji alisema kuwa hakudhamiria kuwaua watoto hao ila mtoto wake alijenga urafiki na kundi la watoto wenye viburi na aliona mwisho wa mtoto wake hautokuwa mzuri, alijitahidi kumuonya lakini hakuna kilichobadilika.

David Conley exits the 183rd District Criminal Courtroom after his arraignment in Houston, Texas August 10, 2015. REUTERS/Daniel Kramer

David Conley akiwa Mahakamani.

>>>“walikuwa wanaelekea pabaya, walikuwa hawana heshima, walikuwa waonevu kwa wototo wenzao… hata Biblia inasema waheshimu baba na mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi kwenye ardhi ya bwana MUNGU wako, lakini hawa hawakutii hii amri na sisemi niliwaua kwa sababu hii ila walikuwa hawana nidhamu… Bibilia inasema usipowaheshimu wakubwa  siku zako zitakuwa fupi duniani”. <<< Hii ni sehemu ya alichokijibu David Conley Mahakamani.

daviD22

Kesi ya David imepangwa kusikilizwa tena September 15 ila mpaka sasa mawakili wanaomsimamia hawajui utetezi wake usimamie upande gani, kwamba alikuwa na kichaa cha muda ama ana matatizo ya akili!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments