Michezo

Mambo ni hiviiiii !!!! Uwanja wa Taifa DSM dakika 120 kabla ya game

on

Weekend hii imebeba siku kubwa kwa Taifa la Tanzania upande wa Michezo ambapo jana March 23 2019 ilisubiriwa kwa ajili ya pambano la Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo akipigana na Bondia wa Argentina Sergio ambapo Hassan alimshinda kwa kumtwanga K.O kwenye round ya 5.

Leo ni zamu ya Taifa Stars vs Uganda na imekua mechi yenye msisimko sana, Watu mbalimbali maarufu wakiongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim na Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda wametumia muda wao mwingi wa zaidi ya siku 7 kuhamasisha Watu wajitokeze kuipa nguvu Stars.

Hizi ni picha nne kutoka Uwanja wa Taifa ambazo zilipigwa dakika 180 kabla ya muda wa mechi kuanza, watu wamejitokeza kwa wingi na wanaendelea kumiminika uwanjani mpaka sasa.


VIDEO: ANGALIA MWAKINYO ALIVYOENDELEZA UBABE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

PICHA 21 ZA BONDIA MWAKINYO ALIVYOMSHUGHULIKIA MUARGENTINA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments