Michezo

Cheki Mchongo walioutoa TFF unaokuhusu wewe mbunifu.

on

spotsInawezekana ukawa una ubunifu wako lakini ukawa unashindwa wapi utaupeleka na kupata pesa halali ya Kitanzania sasa mchongo huu hapa ambao wameutoa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwakaribisha wabunifu.

Unachotakiwa kufanya ni kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa zitakazokuwa zikitumiwa kwa mechi za nyumbani na ugenini na ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.

Mkwanja walioutoa kwa Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja),ukimaliza unaweza kuwatumia kwenye email yao info@tff.or.tz.

 

 

Tupia Comments