Michezo

Kama ulikuwa unajua soka la wanawake limetupwa, TFF wamefikia hapa Feb 23 2016

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF February 23 limefanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kuingia mkataba na Karibu Tanzania Association kwa ajili ya maendeleo ya soka la wanawake ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kuwa nyuma kwa upande wa Tanzania.

DSC_0073

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Mia walipokuwa wakiongea mbele ya waandishi wa habari

Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wameingia makubaliano na katibu wa TFF Selestine Mwesigwa na kusaini mkataba na Mia Mjengwa ambae ni mshauri wa Karibu Tanzania Association.

DSC_0084

Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisaini mkataba

Mkataba huo ni endelevu na mafunzo ya soka yataanza kutolewa kwa shule za kijamii. Baada ya kumalizika kwa mkutano huo Rais wa TFF Jamal Malinzi aliomba watu kuwa watulivu na kusubiri hadi March 20 ndio kesi ya tuhuma za upangaji wa matokeo kwa michezo ya mwisho ya mechi za Ligi daraja la kwanza itasikilizwa.

DSC_0081

Mshauri wa KTA Mia Mjengwa akisaini mkataba

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Tupia Comments