Michezo

Hili ni tamko la TFF kuhusu tiketi za Ki-elektoniki.

By

on

DSC_0104Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo limetangaza kusitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika tathmini ya kina kabla ya kuendelea tena.
Akitangaza uamuzi huo Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura amesemaUamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya kikao kati ya Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB kilichofanyika jana (Februari 3 mwaka huu) katika ofisi hizo za Shirikisho la soka.
Tathmini hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa ikiwa ni hadhari iliyotolewa na vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea uwanjani kutokana na kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.
Tayari zipo changamoto za wazi ikiwemo uelewa wa washabiki wa jinsi ya kununua na kutumia tiketi hizo, milango michache ya kuingilia uwanjani na washabiki wengi kununua tiketi dakika za mwisho hivyo kuchangia misongamano.
Source:salehjembe

Tupia Comments