Ni good news nyingine kwa maendeleo ya soka la Tanzania, baada ya vyombo vingi vya habari Tanzania kupigia kelele suala la baadhi ya vilabu vya soka Tanzania kushindwa kufanya vizuri kutokana na kutokuwa vizuri kiuchumi kiasi cha kudaiwa kuuza mechi. September 22 kupitia kwa Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ametangaza kuingia mkataba wa udhamini wa Ligi daraja la kwanza na kampuni ya ving’amuzi.
Malinzi amefanunua kuwa mkataba wa Ligi daraja la kwanza unahusisha udhamini wa timu zote 24 kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara, Malinzi amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya milioni 900 za kitanzania na mkurugenzi wa kampuni ya ving’amuzi Lanfang Liao na wiki ijayo utasainiwa mkataba mwingine wa haki za matangazo ya Tv ili Ligi daraja la kwanza ionyeshwe katika TV kama ilivyo kwa Ligi Kuu Tanzania bara.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya ving’amuzi Lanfang Liao amethibitisha kuwa Ligi daraja la kwanza mara baada ya kusaini mkataba wa haki za matangazo ya TV watapata nafasi ya kuonekana katika nchi 14. Baada ya kusaini mkataba wa haki za matangazo ya Tv, vilabu shiriki vya Ligi hiyo vitapewa jumla ya Tsh milioni 15 kwa kila klabu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE