Michezo

TFF imebadili Ratiba ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, sababu ni hii hapa…

on

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kubadili tarehe ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara… TFF imefanya maamuzi hayo kufuatia kubadilishwa kwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na jukumu la kuifundisha Timu hiyo akapewa Charles Borniface Mkwasa.

Ligi Kuu Tanzania ilikuwa ianze August 22 2015 lakini kwa sasa itakuwa hivi, Ligi itaanza Septemba 12 2015 kwa lengo la kumpa muda wa kutosha Kocha Mkwasa wa kukinoa kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza na timu ya taifa ya Nigeria Septemba 5.

download

Mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) ambao utazikutanisha timu za Yanga na Azam FC utapigwa August 22 badala ya August 15 kama ilivyokuwa imetangazwa awali.

Ratiba ya Ligi Kuu sasa inafanyiwa marekebisho na mechi zitakuwa zinachezwa katikati ya wiki na siku za weekend kasoro Oktoba 25 2015 ambapo hakutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu wowote ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge Tanzania.

Boniface-Wambura1-2

Klabu zinazoshiri Ligi hiyo zimeandikiwa barua kupewa taarifa hiyo na wamiliki wa viwanja wameandikiwa barua kukarabati viwanja hivyo ili viweze kukidhi vigezo vya kutumika katika michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza vinginevyo havitaruhusiwa kutumika.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments