Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill mkoani Iringa wameanzisha utalii wa michezo ya magari katika shamba hill kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kutangaza utalii wa ndani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyofanya kwenye Flamu ya Royal Tour.
Akizungumza wakati wa kutangaza kwa mashindano ya magari katika shamba la miti la Sao Hill, Mhifadhi mkuu wa shamba hilo Lucas Sabida alisema kuwa wamejipanga kuanzisha utalii katika shamba hilo ambao utaongeza kipato kwa wananchi na shamba hilo.
Sabida alisema kuwa kwa sasa wameanzisha utalii wa mchezo wa magari ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 11/09/2022 katika shamba la miti la Sao Hill na wananchi wote wanakaribishwa kwenda kutazama mchezo huo.
Alisema kuwa lengo kubwa ni kuanzisha mashindano makubwa ya mbio za magari Africa kwa kuwa wanabarabara ambazo zinahimili hilo na zina urefu wa KM 15000.
Sabida alisema kuwa SAO HILL MISITU AUTO CROSS ni zao jipya la Utalii ndani ya Shamba la Miti SaoHill Mafinga TFS wanasema utalii wa aina hii ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya Shamba la Miti SaoHill