Michezo

Barcelona mambo magumu, waziacha point tatu kwa Granada

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania usiku wa September 21 2019 ililazimika kuifuata Granada ili kucheza mchezo wao wa 5 wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama LaLiga, game hiyo ambayo nahodha wao Lionel Messi aliingia kipindi cha pili akitokea benchi haikuwa rahisi kwa FC Barcelona tofauti na matarajio ya wengi katika mitandao ya kijamii.

Barcelona wakiwa wameshacheza michezo itatu LaLiga hadi sasa, wamejikuta wakipigwa 2-0 dhidi ya Granada magoli yakiwekwa wavuni na Ramon Azeez dakika ya 2 na Alvaro Vadillo dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati baada ya Arturo Vidal kusababisha penati akitokea benchi na kuigharimu yake, huo ni mchezo wa pili wa LaLiga kwa FC Barcelona kupoteza msimu huu kati ya mitano.

Ushindi huo kwa Granada unawafanya wafikishe jumla ya point 10 na kukaa kileleni mwa msimamo wa LaLiga kwa tofauti ya magoli ya kushinda na kufungwa dhidi ya timu za Sevilla na Atletico Madrid walizolingana nazo point 10, Barcelona baada ya kupoteza katika mchezo huo wa ugenini wanaendelea na rekodi yao ya kutopata ushindi LaLiga ugenini toka April 2019.

VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016

Soma na hizi

Tupia Comments