Michezo

Usiku wa Champions League umeisha kimaajabu, tunasubiri Europa League

on

Baada ya mchezo wa UEFA Champions League usiku May 8 na 7 kuwa wa staili ya aina yake, na kupelekea fainali timu mbili za England kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008, usiku wa leo Chelsea na Arsenal watacheza michezo ya marudiano katika nusu fainali ya EUROPA huku wakiwa na matumaini ya kucheza fainali nyingine ya waingereza mwisho wa mwezi huu.

Mara ya mwisho timu za England kukutana kwenye fainali ya EUROPA League (kipindi hicho UEFA Cup) ilikuwa mwaka 1972, ambapo Wolverhampton Wanderers walicheza dhidi ya Tottenham Hotspur na Spurs kushinda 3-2 baada ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini, wakati huo mfumo huo ndio ulikuwa unatumika.

Miaka 47 baadaye, Chelsea na Arsenal wana nafasi ya kufanya hivyo na kuandika historia nyingine tena, itakuwa ni mara ya kwa timu za jiji moja kugombania Ubingwa wa Ulaya katika fainali, mara ya kwanza walikuwa mahasimu wa jiji la Madrid, club za Atletico Madrid na Real Madrid.

Arsenal wanasafiri kuelekea Valencia wakiwa wanaongoza kwa 3-1, huku Chelsea watakuwa nyumbani baada ya kupata goli la ugenini katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare 1-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt, Kocha wa Arsenal Unai Emery, ambaye alishuhudia matumaini ya timu yake kushiriki ligi ya mabingwa mwakani yakiyeyuka baada ya timu yake kulazimishwa sare na Brighton katika Ligi hiyo ndio nafasi yake pekee ya kucheza Champions League.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang anatamani kucheza na Eintracht Frankfurt kwenye fainali, kuliko kucheza na mahasimu wao, Chelsea. “Siwataki Chelsea, tunawafahamu ni timu nzuri lakini nadhani sisi tutaingia fainali kwanza na ningependa tucheze dhidi ya Frankfurt kwa sababu Chelsea tumeshacheza nao [kwenye ligi]. Nafahamu Frankfurt ni wazuri sana kama sote tutaingia fainali utakuwa mchezo mzuri sana”

Kocha wa Chelsea alizomewa na mashabiki wao kwenye mapumziko katika mechi dhidi ya Watford Jumapili iliyopita, lakini walirudi vizuri kipindi cha pili na kushinda kwa mabao 3-0 na kujihakikishia nafasi ya nne kwenye msimo wa ligi ila leo wanashuka uwanjani kucheza dhidi ya Frankfurt watatoka? game zinaoneshwa ST World of Football.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments