Hivi karibuni Rapa Nay wa Mitego aliachia wimbo ‘Moto’ ambao baadhi ya mashairi ya wimbo huo yanadaiwa kuwagusa baadhi ya wasanii akidai wamepoteza mwelekeo kwenye ramani ya muziki na kwamba kuna mahali walikosea, hivyo wajirekebishe.
Sasa leo July 5, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM, mmoja kati ya wasanii wanaodaiwa kutajwa kwenye wimbo huo Young Killer amefunguka akiielezea mistari hiyo akisema Nay wa Mitego ameelemea upande mmoja kwenye wimbo wake na hakupaswa kusema Baraka de Prince anahemea mipira wakati amezunguka kwenye Fiesta kuliko Nay wa Mitego.
>>>“Kitu kinachokuja kutokea kwenye maisha mimi naamini njia nyepesi ni ile iliyonyooka peke yake. Kaka zetu muda mwingine wawe wanachukua time yao na kutuelewesha sisi wadogo zao kabla ya kutuweka hadharani katika hali ya ubaya.
“Nikimzungumzia Ney Wa Mitego, ukianza kusikiliza ngoma yake kwa mara ya kwanza, niliona kabisa ameelemea upande umoja. Huwezi kumzunguzia Baraka anahemea mipira wakati mwaka jana amefanya Fiesta nyingi kuliko yeye. Ukiangalia, Baraka muda huo ana wimbo Top 20 na wewe huna ngoma halafu unasema anahemea mipira.
“Kwa hiyo, unaona brother amevunja heshima. Unamuweka sawa kwa sababu madini yanawepo na mistari hujui pa kuipeleka. Ni kama kuwa na nguo ya ndani ya Milioni umeiweka ndani hakuna anayeiona.” – Young Killer.
Mbali na hayo Young Killer amezungumzia wimbo wake mpya alioutambulisha leo kwenye kipindi hicho ambao amemshirikisha Harmonize akisema yeye hayuko Wasafi lakini anafanya nao kazi kwa karibu zaidi.
>>>“Mimi sipo Wasafi ila ni Kundi ninalofanya nao kazi kwa ukaribu zaidi kwa sasa ndio maana unaona wapo hapa ndani. Kwanza kabisa tunamshukuru Mwenyezi Mungu, ujue wasafi ni label kubwa na Mwenyezi Mungu kaibariki iwepo sehemu ambayo ipo kutokana na ina moyo wa kuweza kusaidia kutokana na wao wanvyoona iko sahihi.
“Ukiwa na kipato kidogo na unatumia kikubwa ipo siku utapata kikubwa na kutumia kidogo. Kwa hiyo, namshukuru sana Harmonize ni moja ya watu walioamua kufanikisha kazi hii pamoja na uongozi wake wa Wasafi kunipa ushirikiano mpaka video.
“Ngoma inaitwa Unaionaje lakini mwanzoni, wakati naandika wimbo nilipenda iitwe Kunja kwa sababu ilikuwa inazungumzia watu wenye chuki lakini kiitikio kikaleta jina la Unanionaje ambacho kilitoka kwa Harmonize.” – Young Killer.
VIDEO: Diamond Platnumz alivyo perfom Goma nchini Congo