Habari za Mastaa

The Game kwenye headlines ashitakiwa tena, time hii kwa kosa hili hapa…

on

LOS ANGELES, CA - OCTOBER 04:  Jayceon Terrell Taylor aka The Game attends The Game Album Release Party For "Year Of The Wolf" on October 4, 2014 in Los Angeles, California.  (Photo by Gabriel Olsen/Getty Images)

Msanii wa Hiphop Marekani The Game anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani baada ya kushitakiwa kwa kumdhalilisha mwanadada Priscilla Rainey kwenye reality show yake ya “She’s Got Game”.

Mwanadada huyo amefungua mashitaka hayo kwenye Mahakama ya Illinois Federal Court akidai msanii huyo alimfanyia vitendo  vya kumdhalilisha tarehe 2 May mara baada ya kumaliza shooting ya reality show yake.

the game

Documents zilizowasilishwa Mahakamani zinadai kuwa wakati wakiwa kwenye shooting ya scene moja kwenye club ya michezo, The Game alikuwa amelewa pombe na madawa ya kulevya mwanzo mwisho wa shooting hiyo.

Priscilla ameongezea kwa kusema kwamba wakati wanamalizia shooting hiyo mida ya usiku The Game alimfanyia vitendo vya kumdhalilisha ikiwa kulazimisha kupeleka mkono wake chini ya nguo aliyokuwa ameivaa kwa nia ya kumchezea makalio na sehemu zake za siri.

the-game-2

Kesi hiyo inasubiri kusikilizwa mbele ya Mahakama Illinois, na mwanadada huyo anadai fidia ya dola Mil.10,000,000 ( zaidi ya Bilioni 20 za Tz).

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments