Habari za Mastaa

The Game kalipwa pesa na hakutokea kwenye show… Mahakama haijamwacha hivihivi!

on

Msanii wa muziki wa HipHop, The Game amejikuta matatani baada ya promoter kwenda Mahakamani na kufungua kesi ya madai dhidi yake.

Kwa mujibu wa kampuni ya Dream Team Entertainment, LLC, rapper huyo kutoka Compton  aliingia makubaliano na kampuni hiyo ya kwenda kutoa show kwenye Tamasha la Kentucky Derby tarehe 30 October 2014 lakini The Game hakutokea licha ya kulipwa advance ya zaidi ya milion 20.

GAMESHOW4

Kampuni ya Dream Team badaae ilijaribu kudai pesa ya advance waliotoa irudishwe ikiwemo na fine ya pesa iliyotokana na The Dream kuvunja makubaliano ya kutoa show lakini management ya The Game ilikaa kimya na wala hawakuwahi kurudishiwa wala kupokea pesa yoyote toka kipindi hicho.

Rapper Jayceon Terrell Taylor, known by his stage name "Game" and "The Game", sits courtside as he watches the Los Angeles Lakers play the Houston Rockets during their NBA basketball game in Los Angeles, California, November 18, 2012. REUTERS/Alex Gallardo (UNITED STATES - Tags: SPORT BASKETBALL ENTERTAINMENT) - RTR3ALH5

Kesi ikaenda Mahakamani na Mahakama ilitoa namna ya kuumaliza mgogoro huo lakini badala ya The Game kutokea Mahakama, rapper huyo aliamua kupuuzia wito wa Mahakamani… kitendo hicho kimesababisha Mahakama husika kutoka hukumu dhidi ya The Game na kumuamrisha kulipa fidia za hasara zote zilizoingiwa na Dream Team Entertainment, LLC ambapo jumla ya fidia hizo ni zaidi ya bilion 1 kwa pesa ya Kitanzania!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments