Michezo

FC Barcelona wailaza Villarreal, Messi kashindwa kumaliza mechi

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania usiku wa September 24 2019 ilikuwa Nou Camp kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu nchini Hispania dhidi ya Villareal, mchezo huo ulikuwa na ushindani kapokuwa Villarreal walipoteza kwa magoli 2-1.

Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 6 na Arthur Melo dakika ya 15 ya mchezo, wakati goli pekee la Villarreal likifungwa na Santi Cazorla dakika ya 44 ya mchezo, hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa presha kuhusu hali ya staa wa FC Barcelona Lionel Messi.

Messi katika mchezo huo alitolewa dakika ya 46 na kuingia Ousmane Dembele baada ya dakika za kwanza kumalizika akiwa na majeraha, Messi huu ndio ulikuwa mchezo wake wa kwanza wa msimu kupata nafasi ya kuanza 2019/2020 lakini amemaliza kwa kutolewa hali ambayo imeanza kuleta hofu kuwa staa huyo kaumia jeraha jingine au kajitonesha.

VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”

Soma na hizi

Tupia Comments