Michezo

“Thierry Henry ghafla alizima TV” Evra

on

Mchezaji wa zamani wa Man United Patrice Evra amefunguka kuwa Mchezaji mwenzake wa Ufaransa na legend wa Arsenal Thierry Henry aliwahi kumualika nyumbani kwake waangalie nae game ya Arsenal lakini alizima TV mara tu baada ya kuona Granit Xhaka kapewa kitambaa cha unahodha.

“Thierry Henry alinialika nyumbani kwake tuangalie game ya Arsenal, nilienda ila Thierry Henry ghafla alizima TV na kuniambia samahani siwezi kuangalia Xhaka anakuwa nahodha wa klabu yangu”>>> Patrice Evra

Kauli hiyo ya Evra inakuja muda mfupi baada ya Arsenal kupoteza mchezo kwa kupigwa 1-0 vs Burnley huku Xhaka akiishia kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 56.

Soma na hizi

Tupia Comments