Michezo

Thomas Ulimwengu arudi TP Mazembe

on

Club ya TP Mazembe ya Congo DR imetangaza rasmi kumrejesha katika timu hiyo mchezaji wao wa zamani Thomas Ulimwengu aliyeondoka katika club hiyo 2016.

Ulimwengu mwenye umri wa miaka 27 anarejea TP Mazembe kwa mkataba wa miaka miwili, Mazembe wanamrejesha Ulimwengu baada ya safari yake ya soka Ulaya kutokuwa nzuri na kuamua kurejea Afrika.

Baada ya Ulimwengu kuondoka Tanzania na kwenda Ulaya alienda kuanza maisha yake kwenye club za AFC Eskilstuna ya Sweden, Skloboda katika kipindi cha 2017-2018 na baadae akaamua kurejea Afrika katika club ya JS Saoura ya Algeria.

Soma na hizi

Tupia Comments