Michezo

Ronaldo kaanza kumshawishi naodha wa Ajax Matthijs de Ligt

on

June 9 2019 ilichezwa fainali ya UEFA Nations League kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ureno dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi, mchezo huo wa fainali ulimalizika kwa Ureno kutwaa taji la Nations League kwa kuifunga Uholanzi kwa goli 1-0.

Baada ya game Cristiano Ronaldo alionekana akiongea na nahodha wa Ajax aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Uholanzi Matthijs de Ligt, baada ya mchezo wengi walitaka kufahamu Ronaldo alikuwa akiongea nae nini mchezaji huyo, ndio ikabahinika kuwa ameshawishi aende Juventus.

“Ronaldo aliniomba niende Juventus nilishangazwa na ombi lake ndio maana nilianza kucheka, sikuweza kumuelewa kwa mara ya kwanza, naenda mapumziko kwa sasa na nitafikiria ni kitu gani bora kwangu halafu nitaamua, ni muhimu kwa mchezaji mdogo kupata nafasi ya kucheza hicho ndio nataka nijiridhishe nacho”>>>Matthijs de Ligt.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments