Michezo

DONE DEAL: Shiza Kichuya kasaini Misri

on

Winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea club ya Simba SC Shiza Ramadhan Kichuya tayari amekamilisha usajili wa kujiunga na club ya Pharco inayoshiriki Ligi daraja la pili Misri.

Kichuya amejinga na Pharco ya Misri lakini baada ya kukamilisha usajili huo ametolewa kwa mkopo katika club ya Enppi inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri, uhamisho wa Shiza Kichuya umekamilishwa wakati huu mchezaji huyo akiwa kaenda Alexandria Misri kucheza mchezo wake wa CAF Champions League.

Kwa maana hiyo sasa baada ya Shiza Kichuya kukamilisha usajili huo na ITC yake kutarajiwa kutumwa, hatutomuona katika kikosi cha Simba SC kitakachocheza mchezo wa tatu wa hatua ya Makundi dhidi Al Ahly CAF Champions League.

Kichuya sasa atapata fursa na kuungana na watanzania wenzake katika Ligi Kuu Misri ambao ni Himid Mao anayecheza Petrojet aliyojiunga nayo akitokea Azam FC na Yahya Zayd aliyejiunga na Ismaily akitokea Azam FC pia, timu ya Kichuya ENNPI kwa sasa ipo nafasi ya 14 ikiwa na point 21.

Msimamo wa Beno Kakolanya Yanga ndio huu, katuma tena barua

Soma na hizi

Tupia Comments