Habari kubwa kwa sasa katika soka la bongo ni kuhusu aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha kutangaza kujiuzulu nafasi yake, wengi walikuwa wanaripoti kuwa katibu mkuu huyo katangaza kujiuzulu kwa shinikizo na sio maamuzi yake, kitendo ambacho kilifanya mchana wa January 23 wapenzi na wanachama wa klabu hiyo wakusanyike makao makuu na kupinga uamuzi huyo katikavyombo vya habari.
Kwa upande wa Dk Jonas Benedict Tiboroha ameeleza sababu ya kujiuzulu ni yeye mwenyewe kaamua wala sio shinikizo, sababu kubwa iliyomfanya Tiboroha ajiuzulu ni kuongezewa majukumu ya uhadhiri wa chuo kikuu Dar Es Salaam, kitu ambacho kimemfanya aachane na nafasi yake hiyo Yanga.
“Ukweli nimejiuzulu kwa makubaliano tu kwa sasa nipo busy na kazi zangu, kiukweli watu wanapaswa kujua kuwa mimi ni mhadhiri na shughuli zangu, mwenzetu mmoja atakuwa hayupo, kwa hiyo nimeongezea majukumu na muajiri wangu ambao ni chuo kikuu DSM, hivyo siwezi kumudu kuendelea kuongoza Yanga” >>> Tiboroha
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.