Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: TIC yakutana na brela, TRA, Uhamiaji kujadili fursa za uwekezaji
Share
Notification Show More
Latest News
Maneno ya Manara kuelekea Mchezo wa Yanga na Simba leo, “Nendeni mkapiganie Jezi na jina la Club’
August 13, 2022
Video: Mo Dewji alivyokutana na Wachezaji wa Simba, kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
August 13, 2022
Picha: Kinachojiri kwa Mkapa kwenye mechi ya Watani wa jadi ‘Simba na Yanga’
August 13, 2022
Kizz Daniel alivyopanda jukwaani na bendera ya Tanzania, Watanzania wamsamehe kwa yale yaliyotokea
August 13, 2022
Video: Hamisa Mobetto aonesha gari jipya alilonunuliwa na mpenzi wake
August 13, 2022
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > TIC yakutana na brela, TRA, Uhamiaji kujadili fursa za uwekezaji
Top Stories

TIC yakutana na brela, TRA, Uhamiaji kujadili fursa za uwekezaji

April 30, 2022
Share
2 Min Read
.
SHARE

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimekutana na wakuu wa Taasisi zinazounda huduma ya mahala pamoja ili kuendelea kujadili mikakati ya uboreshaji wa huduma kwa wawekezaji. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu mjini Morogoro.

Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA amesema majadiliano yalikuwa juu ya namna bora ya kufanya maboresho ya Mfumo wa huduma kwa wawekezaji kupitia dirisha la mahala pamoja “One Stop Facilitation Center”. Mkutano huu unawakutanisha Wakuu wa Taasisi kwa ajili ya kuboresha mfumo huo wa uwekezaji mkoani Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya kuimarisha sekta ya uwekezaji nchini.

.

“Kukamilika kwa maboresho ya Mfumo wa Uwekezaji unaohusisha Taasisi mbalimbali zinazosimamia Sekta ya Uwekezaji hapa Nchini, kutachagiza ukuaji wa sekta hiyo”. amesema Nyaisa.

Ameongeza kwa kusema kuwa, matarajio ya kutumia mfumo huo ni kuongeza idadi ya wawekezaji na kukuza uchumi pamoja na kupunguza mizunguko ya mchakato wa ukusanyaji wa taarifa za mwekezaji, ili kukabiliana na hali ya wawekezaji kuomba nafasi ya kuwekeza kwenye mataifa mengine ya jirani.

.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma kwa Wawekezaji Ndg. John Mnali amesema kukutana kwa Taasisi zinazohusika na utoaji vibali mbalimbali kwa wawekezaji ikiwemo sekta ya ardhi kutarahisha kupunguza malalamiko ya ucheleweshaji wa vibali hivyo, ambapo kwasasa zoezi zima litafanyika kwa njia ya mtandao, lengo ni mchakato wa uratibu wa taarifa kukamilika kwa siku moja.

“Mwanzoni ilikuwa ikiwachukuwa wawekezaji mpaka siku saba au hata na zaidi kupata vibali hivyo lakini sasa kuna mabadiliko makubwa na lengo letu ni Mwekezaji aweze kupata vibali vyote kwa siku moja kama atakuwa amekamilisha nyaraka zote zinazohitajika”, amesema Mnali.

Kikao hicho cha majadiliano ya kuboresha mfumo wa uwekezaji kimehusisha Wakuu wa Taasisi mbalimbali ikiwemo Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA), BRELA, Uhamiaji, Wizara ya Ardhi, TMDA, NEMC, TBS, TANESCO, pamoja na TNBC.

You Might Also Like

Mauaji Moro: Mume amnyonga Mkewe na mtoto, Kaka wa Marehemu afunguka

Basi la New Force latumbukia korongoni, Mmoja afariki, Polisi anena chanzo

Ndugu abiria kulipwa Milioni 150, Wakili aibua mapya ‘Watu binafsi waliopost meme wajiandae’

Ajali Mbaya!! Watu sita wafariki, Polisi wafunguka, chanzo ‘Dereva alikuwa Mwendokasi, lilipinduka’

Hafla ya makabidhiano ya data za utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia kwa vitalu Zanzibar

Edwin TZA April 30, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo April 30, 2022
Next Article Utata Temeke: Meya, Madiwani wataka eneo lao, Mkurugenzi apewa maagizo (video+)
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Maneno ya Manara kuelekea Mchezo wa Yanga na Simba leo, “Nendeni mkapiganie Jezi na jina la Club’
Sports August 13, 2022
Video: Mo Dewji alivyokutana na Wachezaji wa Simba, kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
Sports August 13, 2022
Picha: Kinachojiri kwa Mkapa kwenye mechi ya Watani wa jadi ‘Simba na Yanga’
Sports August 13, 2022
Kizz Daniel alivyopanda jukwaani na bendera ya Tanzania, Watanzania wamsamehe kwa yale yaliyotokea
Entertainment August 13, 2022

You Might also Like

Entertainment

Video: Hamisa Mobetto aonesha gari jipya alilonunuliwa na mpenzi wake

August 13, 2022
Entertainment

Huyu ndie Kizz Daniel, Bilionea wa Buga, Mikasa ya Polisi mpaka kupelekwa Mahakamani

August 12, 2022
Entertainment

Nandy ametuletea hii video mpya ya wimbo wake akiwa na Oxlade ‘Napona’

August 11, 2022
Entertainment

Meneja wa Diamond ‘Sallam’ atia neno baada ya Kizz Daniel kuwaomba radhi watanzania

August 10, 2022
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?