Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) baada ya jana kutoa tiketi 100 za VIP kwa mashabiki wa Simba SC wanawake wataokwenda uwanjani kuangalia game ya Simba dhidi ya Vipers SC ya Club Bingwa Afrika.
Leo pia ZIC imetoa tiketi 100 za VIP kwa ajili ya mashabiki wa Yanga wanawake wataokwenda uwanjani kuisapoti Yanga kesho uwanja wa Mkapa dhidi ya Real Bamako ya Mali mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Kila mwaka March 8 2023 duniani kote huadhimisha siku ya Wanawake duniani na kwa Tanzania, ZIC wameamua kusherehekea siku hiyo kwa kugawa tiketi kwa mashabiki wa Simba na Yanga Wanawake.