Michezo

Unaambiwa tiketi za kielektorinik leo zimegoma kufungua milango mkwakwani.

By

on

tiketi za electronic 2Leo Tiketi za elektronik zimeshindwa kufungua milango ya elektronik kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kuzua tafrani kubwa,Kawaida mashabiki huzitumia tiketi hizo kufungua mlango lakini unaambiwa kila walipojaribu leo ilishindikana na kusababisha zogo kwa waliokuwa wanataka kuingia uwanjani.
Uwanja wa Mkwakwani uliopo Jijini Tanga umefurika mashabiki waliojitokeza kushuhudia mechi hiyo iliyokuwa inachezwa kati ya wenyeji Coastal Union dhidi ya mabingwa Yanga.
Kutokana na hali hiyo ililazimu utaratibu wa kawaida uanze kutumika kwa mashabiki kuingia na tiketi kuchanwa kama kawaida, kitu ambacho hakikuwa kimepangwa.
Source:Salehjembe.

Tupia Comments