TikTok imewahakikishia malipo kwa wafanyakazi wake wa Marekani hata kama Mahakama ya Juu haitabatilisha sheria ambayo italazimisha uuzaji wa programu hiyo au kuipiga marufuku, uongozi wa kampuni hiyo ulisema kulingana na shirika la habari la Reuters.
“Siwezi kusisitiza vya kutosha kwamba ustawi wako ni kipaumbele cha juu, na kwa hivyo muhimu zaidi, nataka kusisitiza kwamba kwa wafanyikazi huko Marekani, ajira, malipo na marupurupu yako ni salama, na ofisi zetu zitabaki wazi, hata kama hali hii haijatatuliwa kabla ya tarehe ya mwisho ya Januari 19,” memo kwa wafanyikazi wa TikTok ilisema Jumanne.
“Timu yetu ya uongozi inabakia kupambana na upangaji wa hali mbali mbali na kuendelea kupanga njia ya kusonga mbele.”
” kampuni hiyo ilisema, na kuongeza kuwa itaendelea kushughulikia hali hiyo ili kulinda wafanyikazi na watumiaji zaidi ya milioni 170 wa TikTok nchini Marekani.
Ikiwa mahakama haitazuia sheria kufikia Jumapili, watumiaji wapya watakaotaka kupakua TikTok kwenye programu ya Apple au Google App Store huenda watapigwa marufuku, lakini watumiaji waliopo wanaweza kuendelea kupata programu hiyo kwa muda.
Jukwaa hilo maarufu sana linamilikiwa na ByteDance yenye makao yake Uchina na lina wafanyakazi 7,000 nchini Marekani.