Habari za Mastaa

Tinashe anaisambaza rasmi ngoma yake mpya ‘Player’ feat. Chris Brown – (Video)!

on

Baada ya kuisogeza kwetu behind the scenes ya video yake mpya, msanii wa muziki wa Pop R&B kutoka Marekani, Tinashe ameamua kuidondosha video ya wimbo wake mpya Player feat. Chris Brown.

Player ni single ya kwanza itakayopatikana kwenye Album mpya ya Tinashe, Joyride, mbali na kushirikiana na Chris Brown kwenye wimbo huu, wasanii wengine wakubwa watakaosikika kwenye Album mpya ya msanii huyo ni pamoja na Max Martin, Dr. Luke, Hit-By, Travis Scott (ambaye pia ndiye aliyehusikia kwenye uandishi wa single hii), Young Thug na wengine kibao.

NASHE4

Alipoulizwa nini kilimsukuma kufanya kazi na Chris Brown, Tinashe alikuwa na haya ya kusema; >>>” Chris Brown ni mtu ambaye ana kipaji kikubwa sana, cha kuimba na cha kucheza, na nilipomaliza kuingiza vocal zote nikaamua kumtafuta kuona kama angependa kuweka vocal zake pia ili kuifanya track iwe kali zaidi, akakubali”. <<<

NASHE2

Hapa chini nimeisogeza official music video ya Tinashe feat. Chris Brown; ‘Player’ na kama bado video hii haijagusa macho yako basi feel free kuicheki single hiyo hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments