AyoTV

Mambo matano ya kufahamu kama una gari lenye Tinted Tanzania

on

Kazi ya Millard Ayo siku zote ni kukusogeza karibu na matukio yote yanayotokea Tanzania na nje ya Tanzania ambapo ukiwa na APP ya Millard Ayo kwenye simu za Android na IoS utakua unapata notification ya kila mpya ninayoiweka.

Sasa juzi nilipigiwa simu na mtu yuko Arusha akasema Polisi wamemkamata na gari lake sababu lina vioo vyeusi (TINTED) kwenye vioo vya pembeni, mwingine wa Dar es salaam akaniambia amekamatwa sababu ya Tinted ndogo ya kuzuia jua iliyopo kwenye upande wa juu wa kioo cha mbele.

Malalamiko hayo ndio yamefanya nimtafute Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Mohammed Mpinga atufafanulie tujue kabisa nini tunakosea na nini tunapatia.

  1. Kioo cha mbele mwa gari pekee ndio tumekataza kuweka hizo FULL TINTED, hii itasaidia sisi tukisimamisha gari kumuona aliyeko ndani kirahisi na pia kuepusha ajali za Madereva kutoona vizuri.
  2. Pamoja na kukataza Tinted kwenye kioo cha mbele kwenye magari, Tinted ndogo inayopita kama mstari juu kwenye kioo cha mbele ili kuzuia Jua, HAIJAKATAZWA.
  3. Mpaka sasa Polisi haijakataza wala kutoa tamko lolote la kuzuia Tinted kwenye vioo vya pembeni mwa gari hivyo ukisimamishwa hilo sio kosa.
  4. Ni marufuku kuweka Tinted ya mstari chini kwenye kioo cha mbele na kubakisha sehemu tu ya katikati, ni mtindo ambao Mabasi mengi ya abiria yamekua yakiufanya na kuitumia sehemu hiyo ya chini kunadi safari zao.
  5. Hatujakataza Tinted kwenye vioo vingine vya pembeni mwa gari labda kama maelekezo yatakuja baadae…….MTAZAME KAMANDA MPINGA AKIONGEA ZAIDI KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI

VIDEO: Tazama hapa chini Jeshi la Magereza Tanzania lilivyoonyesha uwezo wao na pale Mfungwa anapozingua

Soma na hizi

Tupia Comments