Jeshi la Polisi Tanzania limewatoa hofu Watanzania juu ya tishio la ugaidi Jijini Dar es salaam na maeneo mengine baada ya taarifa ya tahadhari ya usalama iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Polisi imewahakikishia Wananchi kuwa hali ni shwari.
“Jeshi la Polisi limeiona taarifa jana January 25, 2023 katika baadhi ya Vyombo vya Habari ikiwepo Mitandao ya Kijamii Kuhusu tahadhari kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa Wananchi wao kutembelewa na Watu wengi hapa Tanzania wakiwepo Wageni”
“Jeshi la Polisi Tanzania tulianza kulifanyia kazi taarifa hiyo kwa kina toka iliponza kusambaa, hivyo Wananchi wendelee kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida”
“Aidha pale itakapobainika jambo lenye kutia shaka au atakapo onekana mtu/watu wenye kutia mashaka kutokana na mienendo yao, basi taarifa hizo ziripotiwe kwa haraka ili ziweze kufanyiwa kazi”