fB insta twitter

‘Mwarobaini wa wizi wa bodaboda, magari wapatikana’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari ‘Mwarobaini wizi wa bodaboda wapatikana’

Gazeti hilo limeripoti kuwa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi ‘VETA’ imebuni kifaa cha kudhibiti wizi wa magari na pikipiki za abiria maarufu bodaboda kwa kutumia simu ambapo kwa kutumia kifaa hicho, dereva atakuwa na uwezo wa kuzima pikipiki au gari kwa kutumia simu ya mkononi ambayo namba yake itakuwa imefungwa katika chombo hicho.

Akizungumzia kuhusu kifaa hicho Mwalimu wa Teknolojia ya mwasilliano wa VETA , Valerian Sanga alisema alishirikiana na mwalimu mwenzake wa chuo hicho anayefundisha masuala ya umeme, Christian Brighton kubuni kifaa hicho kilichowachukua miaka miwili.

Sanga alisema kifaa hicho kina GPS na kinatumia mawasiliano ya simu kwa kutumia GSM itakayosaidia kujua sehemu pikipiki au gari lilipo, lakini pia kikimwezesha mmiliki kuzima na kuwasha usafiri wake popote ulipo pia sasa wanafunga kifaa hicho kwa gharama ya sh 400,000 lakini wanatarajia baadaye watakapopata oda nyingi, watapunguza bei.

Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya July 03 2016

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 03 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments