Habari za Mastaa

T.I ana mtazamo gani kuhusu mgombea Urais wa Marekani, Hillary Clinton?

on

CEO kutoka kwenye lebo ya Hustle Gang T.I ameingia kwenye headlines baada interview yake na Dj Whoo Kid kwenye moja ya radio nchini Marekani… akiwa kwenye interview hiyo T.I alizungumzia mipango yake ya kufanya collabo na Usher Raymond, Young Thug na B.O.B pia alizungumzia changamoto alizokumbana nazo kwenye kufanya kazi na rapper Travis Scott.

TIPP3

Baada ya kutumia dakika 12 kuongelea vitu vyote hivyo T.I akaulizwa swali linalohusiana na hali ya Siasa sasa hivi nchini Marekani haswa wagombea nafasi ya Urais nchini humo wakiwemo Donald Trump na Hillary Clinton ambae mume wake Bill Clinton alishawahi kuwa Rais wa Marekani pia…

>>>Sio kwamba nina ubaguzi wa kijinsia ama nini ila kusema kweli siwezi kumchagua mwanamke kuwa kiongozi wa nchi ya Marekani… kwa sababu nawajua wanawake na mara nyingi wanafanya maamuzi yasiokuwa ya msingi kwa kufuata mioyo na hisia zao. Huwa wanafanya maamuzi ya mambo mazito kwa vile wanavyojisikia wakati huo alafu badaae wanasema hawakudhamiria kufanya maamuzi hayo… nisingependa kumchagua mwanamke alafu aje kufanya haya..” <<< T.I.

Baada ya interview hii T.I alishambuliwa na watu mbalimbali wengi wakimuuita mbaguzi wa jinsia, wengine wakisema anachukia wanawake… kila mtu alisema lake!

TIPP

Lakini badaae T.I akaamua kuchua time na kupost kupitia page yake ya Twitter post ya kuomba msamaha kwani amegundua kauli yake ilikuwa sio sawa na hivyo anaomba msamaha kwa wale wote aliowakera.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments