Mix

Rais Magufuli kaandikwa tena na tovuti ya gazeti la Uingereza, ni kuhusu Dec 9.

on

Sasa hivi sio habari mpya tena kuona gazeti au mtandao wa nchi flani maarufu duniani limemuandika Rais Magufuli wa Tanzania, tayari mpaka sasa tumeshaona Magazeti ya Australia, South Africa, Zimbabwe, Kenya, China, Uganda na Uingereza yamemuandika Dr. Magufuli.

December 9 2015 baada ya Rais Magufuli kuchukua headlines za yeye kufanya usafi, The Telegraph (telegraph.co.uk) wameandika mistari ambayo inaonyesha kabisa kitendo cha Dr. Magufuli kuingia mtaani kufanya usafi kimewagusa na ni tofauti na Waziri mkuu wa Uingereza ambaye sio rahisi kumuona au kufanya alichofanya Dr. Magufuli.

Kwenye sehemu ya stori yenyewe wamenukuu mistari ya Rais Magufuli kusema ni aibu kusherehekea siku ya uhuru Tanzania wakati nchi ina Wagonjwa wa kipindupindu ambapo kwenye taarifa hiyo ziliambatanishwa picha zikimuonyesha Rais JPM akifanya usafi.

magu 3

magu 2

Magu 1

TAZAMA VIDEO YA RAIS MAGUFULI AKIFANYA USAFI HAPA CHINI.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, InstagramnaYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments